Connect with us

Makala

Rasmi Pamba Jiji Yaachana na Goran

Uongozi wa Klabu ya Pamba Jiji ya jijini Mwanza umefikia maamuzi ya kuachana na kocha wake mkuu Goran Kopunovic na msaidizi wake Henry Mkanwa kutokana na matokeo yasiyoridhisha katika ligi kuu ya Nbc msimu huu.

Goran tayari ameshapewa taarifa hiyo huku akisubiri baadhi ya taratibu za fidia ili kuondoka nchini huku sasa timu hiyo imekabidhiwa kwa kocha Salvatory Edward ambaye alikua msaidizi wa Goran kabla ya kumtimua na kumleta Henry Mkanwa.

Pamba jiji iliyopanda daraja la ligi kuu msimu huu mpaka sasa imecheza michezo saba ikipata sare nne na kufungwa michezo mitatu ikiwa mkiani mwa msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini.

Pamoja na kuwa na uchumi unaoridhisha ikiwa chini ya Jiji la Mwanza klabu hiyo imekua haipati matokeo sahihi nyumbani na ugenini huku sababu kubwa ikitajwa ni mpasuko uliopo klabuni humo upande wa utawala kutokana na masuala ya udhamini.

Kwa mwenendo wa ligi ulivyo endapo klabu hiyo itashindwa kurejesha makali yake basi inaweza kushuka daraja kutokana na timu nyingi kuwa zimejipanga kupata matokeo msimu huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala