Connect with us

Soka

Pablo Awataka 7 Stars

Kocha mkuu wa klabu ya Simba SC, Pablo Franco Martin amesema kuwa amepeleka maombi kwa kocha wa timu ya Taifa Stars , Kim Poulsen na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kuwaomba wawaondoe wachezaji saba wa Simba kwenye kambi ya Timu ya Taifa,

Kocha Pablo amedai kuwa Simba wana mechi ngumu ambayo ndio fainali kwao dhidi ya US Gendermarine kwa ajili ya kufuzu robo fainali ya kombe la shirikisho hivyo wachezaji hao wanatakiwa kupumzika ili kuweka miili yao fiti kwa ajili ya mapambano ya mchezo huo wa April 03.

Wachezaji wa klabu ya Simba sc walioko katika kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania ni Aishi Manula,Shomari Kapombe,Mohamed Hussein,Jonas Mkude,Mzamiru Yassin,Kibu Dennis na Israel Mwenda ambapo wengi wa wachezaji hao ni wachrzaji wa kikosi cha kwanza ambacho huanza michezo mingi ya ligi kuu na michuano ya kimataifa kikosini humo.

Simba sc inakabiriwa na mchezo mgumu wa kundi D dhidi ya Us Gendamarie ya nchini Niger ambapo klabu hiyo inahitaji kushinda ili kupata tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka