Connect with us

Soka

Ni Yanga Sc Vs Azam Fc Crdb Cup

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kufuzu hatua ya fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo sasa itavaana na Azam Fc katika hatua ya  fainali ya michuano hiyo mchezo ambao utafanyika Juni 2 mkoani Manyara baada ya kuifunga Ihefu Fc kwa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Bao pekee kwenye mchezo huu lilipatikana dakika ya 101 kupitia kwa Aziz Ki baada ya kumalizia pasi murua ya Pacome Zouzoua baada ya kumaliza dakika 90 za kawaida kwa 0-0 na hivyo mwamuzi kuongeza dakika 30 kwa mujibu wa kanuni za michuano hiyo.

Yanga sc inapaswa kumshukuru kipa Djigui Diara ambaye mara kadhaa alifanya kazi ya ziada kuokoa michomo na hatari mbalimbali kutoka kwa mshambuliaji Elvis Rupia sambamba na Morouf Tchakei aliyeshirikiana na Moses Chukwu kukishika kiungo cha Yanga sc.

Aziz Ki hakua na mchezo mzuri licha ya kufunga goli ambapo mara kadhaa alikua akipoteza mipira mara kwa mara huku Kelvin Nashon akifanya kazi ya ziada kumlinda kiungo huyo asilete madhara langoni kwa Ihefu huku kipa Aboubakar Komeiny akifanya kazi ya ziada mara kadhaa kuzuia hatari hizo.

Ihefu Fc inabidi wajilaumu wenyewe kutokana na nafasi ya wazi waliyoipata baada ya beki Ibrahim Hamd kufanya makosa na mpira kumkuta Dennis Mahundi ambaye alikosa utulivu na kushindwa kumalizia na mpira kutoka nje licha ya kuwa alitazamana na kipa Diaara.

Uwepo wa Khalid Aucho eneo la katikati mwa uwanja uliongeza nguvu kwa Yanga sc na kuingia kwa Pacome Zouzou kuliwafanya Yanga sc wawe watulivu hasa eneo la katikati mwa uwanja wakipanga mashambulizi kwa kasi na akili kubwa kiasi hata bao pekee la Aziz Ki lilitokana na utulivu wao.

Yanga sc sasa watavaana na Azam Fc katika mchezo wa fainali ambao unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na upinzani mkubwa baina ya timu hizo ambapo hapo awali katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu Yanga sc ilikubali kipigo cha mabao 2-1.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka