Connect with us

Soka

Man City Mabingwa Epl

Klabu ya Manchester City imetwa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza kwa mara ya nne mfululizo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Westham Fc katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Ettihad jijini Manchester.

Man city ilihitaji ushindi tu ili kuchukua ubingwa huo huku Arsenal ikihitaji ushindi na kumuombea Man City apoteze ama atoe sare ili kuchukua ubingwa huo ambao wameukosa kwa miaka 20 sasa tangu wautwae mwaka 2004.

Mabao ya Phil Phoden dakika ya 2 lilitoa mwanga wa ubingwa huku bao lake la pili katika mchezo huo la  dakika ya 18 liliwafanya Man city kuwa na uhakika wa ubingwa huku Mohamed Kudus akifunga bao la kwanza kwa Westham united dakika ya 42 lakini Rodri aliongeza bao la tatu na la ubingwa kwa Manchester City dakika ya 59 ya mchezo.

Man Cuty baada ya ushindi huo ilifikisha alama 91 za ligi kuu ambapo pamoja na kutwaa ubingwa huo pia wamefuzu michuano ya klabu bingwa barani ulaya huku Arsenal Fc ikishika nafasi ya pili kwa alama 89 na kuungana na timu za Liverpool na Aston Villa kucheza Uefa huku Tottenham akifuzu michuano ya ligi ya Europa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka