Connect with us

Makala

Mzamiru Yupo Sana Simba Sc

Klabu ya Simba Sc imetangaza kumbakisha Mzamiru ndani ya viunga vya Msimbazi kwa miaka miwili ijayo baada ya kukubali kumuongezea mkataba wa miaka miwili utakaodumu mpaka Juni 31 2026.

Mzimiru ameibuka kuwa moja ya wachezaji tegemeo klabuni hapo tangu alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2016 akitokea Mtibwa Sugar ambapo licha ya changamoto za kuletewa mastaa wa kigeni eneo la kiungo Mzimiru hajawahi kuteteleka.

Mkataba wa awali wa kiungo huyo unafikia tamati juni 31 mwaka huu na sasa pamoja na marekebisho makubwa ya kikosi kiungo huyo anaendelea kusalia klabuni hapo ambapo analetewa mastaa wa maana kuja kushindania nafasi.

Eneo la kiungo la Simba sc msimu uliopita lilitawaliwa na Fabrice Ngoma ambaye alikua panga pangua huku Mzamiru Yassin,Sadio Kanoute,Abdalah Hamis wakipishana mara kwa mara eneo hilo.

Mpaka sasa sambamba na mazungumzo kuendelea baina ya klabu hiyo na wachezaji kadhaa wa ndani na nje ya nchi ili wajiunge na klabu hiyo huku ikiwa tayari imemnasa Yusufu Kagoma kutoka Singida Fountain Gate Fc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala