Connect with us

Soka

Msuva Majanga Tupu

Klabu ya JS Kabylie ya Algeria  imetangaza kufikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba wa aliyekua mchezaji wao raia wa Tanzania, Simon Msuva ambapo mpaka sasa sababu ya kuvunja mkataba huo haijawekwa wazi.

Kupitia mtandao wao wa kijamii wa Instagram wa klabu hiyo wameeleza kuwa wamevunja mkataba huo kwa amani na wanamtakia mafanikio mema katika klabu nyingine atakayo jiunga nayo.

Msuva alijiunga na klabu hiyo mwezi Julai mwaka huu ambapo baada ya kuwa ameshinda kesi dhidi ya klabu ya Wydad Casablanca ambayo ilimvunjia mkataba kinyume na taratibu ambapo baada ya kesi huko Fifa klabu hiyo iliamriwa kumlipa staa huyo.

Msuva mchezaji wa zamani wa Yanga sc na Moro United mara ya mwisho kabla ya kujiunga na klabu hiyo timu kadhaa za ndani zilionyesha nia ya kutaka kumsajili lakini staa huyo hakua na mpango wa kurudi hapa nchini na mpaka sasa haijafahamika iwapo yupo tayari kurejea kucheza soka nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka