Connect with us

Makala

Morocco Atema Watatu Zanzibar Heroes

Kocha wa timu ya Taifa ya Zanzibar Hemed Morocco amewatema mastaa watatu katika kikosi cha timu hiyo kilichoingia kambini Disemba 24 kujiandaa na michuano ya Mapinduzi Yanayotarajiwa kufanyika Visiwani humo kuanzia Januari 3 mwaka 2025.

Awali Morocco aliwaita zaidi ya wachezaji 20 katika kambi ya timu hiyo ambapo aliwataka kuripoti kambini Disemba 24 lakini mastaa Abdalah Said Lanso wa Kmc na Ibrahim Mkoko wa Namungo walichelewa kuripoti kambini bila taarifa maalumu hali iliyosababisha kutemwa katika kikosi hicho.

Mastaa hao wamechelewa kuripoti wakati tayari klabu zao zilishawapa ruhusa ndani ya muda muafaka.

Baada ya wachezaji hao kutemwa kocha Morocco alimuita mchezaji Ali Said Mabata kutoka timu ya uhamiaji Fc kuchukua nafasi hiyo.

Ikiwa hilo halijasahaulika kwa wadau wa soka Visiwani humo,Kocha huyo kwa mara nyingine amemuondoka kikosini mchezaji Abdulaaziz Makame Bui wa Klabu ya Geita Gold Fc kutokana na kuchelewa kambini ambapo nafasi yake imechukuliwa na Abubakar Nizar wa klabu ya Azam Fc chini ya miaka 20 pamoja na Abdulnasir Abdalah Casemiro wa timu ya mlandege Fc.

Zanzibar Heroes imejizatiti kufanya vizuri msimu huu katika michuano ya kombe la mapinduzi ambalo linashirikisha timu za Taifa msimu huu na sio klabu kama ilivyozoeleka.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala