Connect with us

Soka

Moloko Atua Libya

Siku chache baada ya kuachana na klabu ya Yanga sc winga Jesus Moloko ameamua kujiunga na klabu ya Al Sadaqa SC Benghazi inayoshiriki Ligi Kuu ya Libya akiungana na aliyekua mshambuliaji wa Simba Sc Jean Baleke kukipiga nchini humo.

Kusajiliwa kwa Moloko nchini humo kumehitimisha tetesi za klabu za hapa nchini zilizokua na mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo ikiwemo Geita Gold Fc ambayo ilikua mstari wa mbele kuhakikisha inamsajili staa huyo wakati wa dirisha dogo la usajili.

Winga huyo sasa atakipiga ligi moja na aliyekuwa mshambuliji wa mshambuliaji wa Simba Jean Baleke ambaye amesajiliwa ya Al Ittihad baada ya TP Mazembe kumtoa tena kwa mkopo na alimalizana na Simba baada ya muda wake wa mkopo kumalizika sasa atakuwa akikiwasha katika klabu hiyo, hadi Januari 30, 2025.

“Muda mchache kabla ya dirisha la usajili kufungwa winga Mkongomani Jesus Moloko atakuwa sehemu ya ngome yetu akitoka Yanga ya Tanzania”Ilisomeka taarifa ya klabu hiyo ambayo ipo nafasi ya nane ya msimamo wa ligi kuu nchini humo ikiwa na alama sita baada ya kucheza michezo tisa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka