Klabu ya Yanga imeendelea na harakati za kuboresha kikosi chake ambapo baada ya kusajili mapro wa kigeni kadhaa sasa imegeukia wazawa pamoja na kuboresha benchi la ufundi.Katika maboresho haya klabu hiyo inamuwania wingi kisheti wa Mtibwa Sugar Salumu Kihimbwa ili akaboreshe winga za klabu ambazo zilikua zinasua sua.
Kihimbwa ni mali ya mtibwa sugar baada ya kusaini mkataba mrefu siku za nyuma hali itakayowalazimu wababe hao wa kariakoo kutoa fungu nene ili kumalizana na Mtibwa ambayo mkurugenzi wake Jamal Byser anasifika kwa kugundua vipaji na kuvikuza kisha kufanya biashara na timu itakayomhitaji.
Winga huyo pia tetesi zinadai anahitajika na mahasimu Zao wa Kariakoo Simba sc hivyo kuwalazimu Yanga kutumia nguvu ya ziada huku ikisemekana ripoti za makocha wote Aussems na Zahera zimemtaja kumhitaji.
Pia Yanga iko karibuni kumalizana na kocha wa Kagera Sugar Mecky Mexime ili kumsaidia Zahera,Kocha huyo aliyeichezea Mtibwa sugar kwa mafanikio nahitajika ili kwenda kuziba pengo la kocha msaidizi kwani aliyepo sasa Noel Mwandila ni mtaalamu wa viungo hivyo atahamishiwa rasmi katika taaluma yake ya viungo.
Endapo mazungumzo hayo yatafanikiwa basi Mexime aliye kwenye hatihati ya kushuka daraja na timu ya Kagera Sugar endapo atapoteza mchezo dhidi ya Pamba ya Mwanza kwenye hatua ya mtoano(Play-off) basi atasaini mkataba wa miaka miwili klabu hapo.
Pia taarifa za ndani zinadai hata kutemwa kwa Deus Kaseke kunasababishwa na kukosekana kwa ufanisi katika eneo la pembeni la fowadi ya timu hiyo hivyo kuongeza mahitaji ya Kihimbwa klabuni hapo.
Kaseke na baadhi ya mastaa wengi mikataba yao inaisha msimu huku taarifa zikidai wengi watatemwa kupisha usajili mkubwa ili kuongeza makali ya kikosi hicho.