Connect with us

Makala

Mbadala ya Zimbwe,Mzamiru Watambulishwa Simba Sc

“Msimu bora Uanze” Ndio kauli inayosikika vijiweni kutokana na usajili kabambe ambao klabu ya Simba Sc imeufanya mpaka sasa ikiwasajili mastaa wa maana ambapo sasa imewatambulisha mabeki Valentino Nouma na kiungo Omary Abdalah.

Wachezaji hao ingawa wamesajiliwa watakua na kazi ngumu ya kufanya ili kupata nafasi ya kuanza kikosini kutokana na ukweli kwamba waliowakuta ambao ni Mohamed Hussein na Mzamiru Yassin wako vizuri na tayari wanauzoefu ndani ya timu tayari.

Nouma ni mzaliwa wa nchi ya Burkina Fasso akiichezea klabu ya Fc Lupopo ya nchini DR Congo ambao licha ya kuwa beki mzuri na anapata namba katika kikosi cha timu ya taifa alilazimika kugawana muda wa kucheza na Chadrack Boka ambaye amejiunga na Yanga sc.

Beki huyo mwenye miaka 24 ya kuzaliwa alijiunga na Lupopo akitokea klabu ya nyumbani kwao Burkina Fasso iitwayo AS Douanes msimu wa 2023 ambapo baada ya msimu mmoja sasa amejunga na Simba sc kwa mkataba wa miaka mitatu.

Kwa upande wa Omary Abdalah yeye ni kiungo ambaye msimu uliopita aliichezea Mashujaa Fc na amesajiliwa pia akiwa na kazi ngumu ya kugombania namba na mastaa wa kigeni waliotua klabuni hapo msimu huu.

Mbali na wachezaji hao tayari Simba sc imewasijili  Abdulrazack Mohamed Hamza (21) kutoka SuperSport United ya Afrika Kusini na Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union.
Wengine ni kiungo wa ulinzi, Mnigeria, Augustine Okejepha (20) kutoka Rivers United ya kwao, Port Harcourt na winga Mzambia, Joshua Mutale (22) kutoka Power Dynamos ya kwao, Kitwe na kiungo mshambuliaji, Débora Fernandes Mavambo (24) mwenye uraia pacha wa Kongo – Brazzaville na Angola kutoka Mutondo Stars ya Zambia.
Wapya wengine ni washambuliaji Mganda, Steven Mukwala (24) kutoka Asante Kotoko ya Ghana na Muivory Coast, Jean Charles Ahoua (22) kutoka Stella Club d’Adjamé ya kwao, Abidjan na mzawa, Valentino Mashaka Kusengama (22) kutoka Geita Gold.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala