Connect with us

Makala

Magori,Ng’ambi Kusimamia Usajili Simba Sc

Bosi wa klabu ya Simba sc Mohamed Dewji ameamua kuwakabidhi faili zima la usajili wa mastaa klabuni hapo kwa gwiji Crescentius Magori pamoja na Mulamu Ng’ambi ili kurejesha furaha kwa mashabiki wa klabu hiyo kutokana na klabu hiyo kutofanya vizuri kwa mwaka wa tatu sasa.

Sababu kubwa ya kufanya ni baada ya kuona kuwa pesa za usajili zinatoka lakini mastaa wanaosajiliwa klabuni hapo hawana viwango vya kuitumikia klabu hiyo hivyo bora kuwarejesha wakongwe hao ambao waliipa Simba sc nyakati za furaha kwa takribani miaka minne mfululizo.

Wawili wataungana na Babrah Gonzalez ambaye anaweza kurejeshwa kama Mtendaji mkuu wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Iman Kajula ambaye ataondolewa mwishoni mwa msimu huu.

Magori ndie aliwasajili mastaa kama Rally Bwallya,Gerson Fraga,Luis Miqquisone,Erasto Nyoni,Aishi Manula na Shomari Kapombe,Pascal Wawa na wengineo ambao waliifanya klabu ya Simba sc itambe kwa miaka minne mfululizo nchini huku ikifika hatua ya robo fainali katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala