Connect with us

Soka

Lyanga Anukia Simba Sc

Uongozi wa klabu ya Simba Sc uwewasiliana na menejimenti ya kiungo wa ushambuliaji wa klabu ya Azam Fc Ayoub Lyanga ili kuangalia Uwezekano wa kuipata huduma yake katika dirisha kubwa la usajili linalotarajiwa kufunguliwa mwezi ujao.

Lyanga ambaye anacheza kama winga wa kushoto ama kulia tayari anaelekea kumaliza mkataba wake mwezi ujao baada ya ligi kuu kuisha mwezi ujao na taarifa za ndani zinasema kuwa anasikiliza ofa kwanza kutoka klabuni kwake Azam Fc kisha ndio ataangalia ofa kutoka klabu zingine.

Kwa hali ya sasa ya kikosi cha Azam Fc Lyanga amekua chaguo la pili nyuma ya Kipre Junior,Gibril Silla na Idd Nado ambapo mara nyingi inampasa kusubiri kuingia kama mbadala ama anaweza asicheze kabisa michezo kadhaa.

Simba sc inaweza kumnasa Lyanga endapo itamuwekea ofa kubwa mezani kuizidi Azam Fc ambapo amekua hapati nafasi ya mara kwa mara kucheza hali ambayo inaweza kumshawishi mchezaji huyo kukubali kuachana na Azam Fc.

Simba sc ipo katika mchakato wa kufanya mabadiliko makubwa kikosini humo kutokana na kutokufanya vizuri kwa misimu mitatu sasa ambapo ubingwa wa ligi kuu umechukuliwa na Yanga sc na timu hiyo kukosa makombe kwa miaka yote hiyo wakiambulia ngao ya jamii pekee.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka