Connect with us

Makala

Lakred Kumpisha Mpanzu Dirisha Dogo

Golikipa wa klabu ya Simba Sc Ayoub Lakred yupo mbioni kuondoka nchini kurudi nyumbani kwao nchini Algeria baada ya klabu hiyo kuamua kuvunja mkataba wake ili kuruhusu usajili mpya klabuni hapo.

Mabosi wa Simba Sc walimsajili kipa Moussa Camara baada ya kugundua kuwa Ayoub ana majeraha ambayo yangechukua muda mrefu kupona huku pia akikabiliwa na uzito mkubwa hali iliyosababisha majeraha hayo.

Baada ya Camara kufanya vizuri langoni mabosi wa timu hiyo waliamua kuvunja mkataba wa Ayoub ili kusajili mshambuliaji ambapo tayari wameshakamilisha usajili wa Ellie Mpanzu ambaye anakuja kuchukua nafasi ya Ayoub katika nafasi za wachezaji wa kigeni.

Tayari Ayoub ameshapewa taarifa hiyo na muda si mrefu anaondoka nchini kurudi nyumbani kwao kwa ajili ya kutafuta timu nyingine baada ya Simba Sc kuvunja mkataba wake klabuni hapo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala