Connect with us

Makala

Kibabage Asaini Yanga sc mpaka 2027

Klabu ya Yanga sc imemsainisha mkataba mrefu wa miaka mitatu staa wake Nickson Kibabage kuendelea kukipiga klabuni hapo baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo akitokea Singida Big Stars ambayo sasa inajulikana kama Singida Fountain Gate Fc.

Kibabage alisajiliwa na Yanga sc kwa mkopo wa msimu mzima ambapo sasa baada ya mkopo huo kuisha klabu ya Yanga sc imeamua kumsajili moja kwa moja baada ya kumalizana na klabu yake ya Singida Fountain Gate Fc.

Beki huyo mfupi mwenye kasi ni mzaliwa wa Morogoro akiwa na uzoefu wa kuitumikia timu ya Taifa ya Tanzania katika ngazi zote za vijana kabla ya kujiunga na Diffaa Hassan El Jadid ya nchini Morocco kisha akarejea nchini kujiuunga na Kmc na Baadae Mtibwa Sugar.

Baada ya kucheza vizuri kwa nusu msimu akiwa na Mtibwa Sugar alipata ofa nzuri na kujiunga na Singida Big Stars (sasa inaitwa Singida Fountain Gate Fc) ambapo ndipo Yanga sc ilimuona na kumsajili kwa mkopo kisha sasa imemsajili moja kwa moja.

Kibabage inampasa kupambana kujihakikishia nafasi ya kuanza mara kwa mara kutokana na klabu hiyo kumsajili beki kutoka Fc Lupopo Chadrack boka kuja kuchukua nafasi ya Joyce Lomalisa Mutambala ambaye mara kwa mara wamekua wakigawana muda wa kucheza klabuni hapo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala