Connect with us

Soka

Kibabage Anukia Simba Sc

Klabu ya Simba sc imeonyesha nia ya kumsajili beki wa Singida Fountain Gate Fc aliyeko katika klabu ya Yanga sc kwa mkopo Nickson Kibabage kuja kuichezea klabu hiyo msimu ujao kumpa changamoto zaidi Mohamed Hussein katika nafasi ya beki wa kushoto.

Simba sc imewasiliana na Singida Fountain Gate kuulizia kuhusu upatikanaji wa mchezaji huyo wakati wa dirisha dogo la usajili ambapo mpaka sasa bado hakuna makubaliano yeyote yaliyofikiwa kwa pande hizo mbili.

“Ishu ya Kibabage kweli Simba wameutafuta uongozi kuonesha nia ya kutaka saini yake, Bado ni mapema sana kuzungumzia lakini nathibitisha ni kweli jambo hilo lipo na sio dhambi, Hakuna muafaka uliofikiwa mpaka sasa, Kama kutakuwa na lolote klabu itatoa taarifa” Alisema msemaji wa Singida Fountain Gate Hussein Massanza kuhusu suala hilo.

Yanga sc ilimsajili beki huyo kwa mkopo wa miezi sita wakati wa dirisha kubwa la usajili msimu uliopita na sasa wameongeza tena miezi sita wakati wa usajili wa dirisha dogo na staa huyo atakaa klabuni hapo mpaka mwisho wa msimu huu huku Yanga sc ikiwa na kipengele cha kumsajili moja kwa moja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka