Connect with us

Soka

Katwila Aitisha Yanga sc

Kocha Zubeiry Katwila ameipa vitisho klabu ya Yanga sc kuwa yuko tayari kupambana katika mchezo wa ligi kuu utakaofanyika siku ya Jumamosi katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es salaam.

Katwila ambaye ni kocha wa zamani wa Ihefu Sc ambapo amewahi kuifunga Yanga sc alipokua kocha wa klabu hiyo mchezo uliochezwa mkoani Mbeya katika uwanja wa Highlanders Estate kwa mabao 2-1 na kuipa kipigo cha kwanza cha ligi kuu msimu huu.

Kuelekea mchezo huo Katwila amesema kuwa ataingia katika mchezo huo kwa lengo la kupambana ili kupata alama tatu.

“Tutaingia kwa kuwaheshimu Yanga Jumamosi na siyo kuwaogopa tunacheza na timu yenye wachezaji 11 kama sisi na changamoto tunayoipitia ni kipindi cha mpito timu nyingi huwa zinapitia nyakati ngumu kama hizi matokeo haya hayanifurahishi, nimeandaa programu nyingine za mazoezi na kuwapa wachezaji muda zaidi wa mazoezi wa kuongeza viwango vyao.”Alisema Katwila

Mtibwa Sugar ipo katika hatari ya kushuka daraja kutokana na kuwa na kiwango kisichoridhisha huku ikiwa katika nafasi ya mwisho ya msimamo wa ligi kuu ikiwa na alama tano pekee katika michezo kumi na mbili ya ligi kuu ya Nbc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka