Connect with us

Makala

Karia Awalinda Mastaa wa Kigeni

Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Wallace Karia ametolea ufafanuzi suala la wachezaji wa kigeni na kueleza kuwa wachezaji wa kigeni wameongeza ushindani kwenye ligi yetu na kuchangia kukua kwa viwango vya wachezaji wa ndani

Rais Karia amesema haya mapema hii leo wakati akizungumza katika tukio la Uzinduzi wa vifaa vipya vya kurushia matangazo ya mpira wa miguu nchini lililofanyika kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam ambapo kwenye maelezo yake amesema kuwa idadi ya wachezaji wa kigeni imesaidia pia timu ya Taifa kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa.

“Tumeamua kusisitiza kubaki na wachezaji wengi wakigeni licha ya watu wengi kutaka wachezaji wakigeni wapunguzwe,mafanikio ambayo tumeyapata ni kwasababu ya uwepo wa wachezaji wakigeni ambao kabla ya wao kuja timu zetu zilikuwa hazifanyi vyema katika michuano ya kimataifa”,Alisema Rais Karia

“Kwa takwimu tulizonazo wachezaji wakigeni hawajafika hawajafika 70 kati ya wachezaji 600 ambao huwa wanashiriki katika ligi kuu,hivyo wachezaji wetu wanatakiwa na wao watoke nje ili wakapate changamoto na sio sisi kupunguza idadi ya wachezaji wakigeni.”Alimalizia Rais huyo ambaye ndie mwenye mafanikio zaidi nchini upande wa soka la wanaume na wanawake

Hivi karibuni ulizuka mjadala kuhusu idadi ya wachezaji wa kigeni nchini ambapo baadhi ya wadau walitoa maoni wakitaka wachezaji hao wapunguzwe huku wengine wakisisitiza kuwa wabaki idadi hiyo hiyo isipokua kwenye mechi wasianze wote.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala