Connect with us

Makala

Guede Aondoka Singida Black Stars

Mshambuliaji wa klabu ya Singida Black Stars Joseph Guede amefikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake na klabu hiyo kutokana na makubaliano ya pande zote.

Guede aliyesajiliwa klabuni hapo akitokea Yanga sc amefanikiwa kucheza mechi sita pekee za ligi kuu mpaka sasa ambapo hajafanikiwa kufunga bao lolote.

Uwepo wa washambuliaji Elvis Rupia,Athur Bada na Victorien Adebayo huku pia kiungo kama Marouf Tchakei ambaye anaweza kucheza kama mshambuliaji wa pili umeonekana kuwatosheleza mabosi wa Singida Black Stars kutohitaji tena huduma ya Guede.

Guede baada ya kuvunja mkataba wake huo sasa anaangalia baadhi ya ofa alizonazo ndani ya bara la Afrika huku pia akihitajika na baadhi ya klabu za bara la Asia.

Mpaka sasa katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini klabu hiyo imefikisha alama 30 ikiwa katika nafasi ya pili ya msimamo ikiwa imecheza michezo 14 ya ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala