Kocha wa klabu ya Yanga Sc Miguel Gamondi amesema kuwa amegundua wapinzani wake wanamuogopa sana kutokana na ubora wake hivyo wamemtengenezea mtego afungwe mechi mbili ili afukuzwe.
Gamondi amesema hayo mapema hii leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alikua akielezea namna timu hiyo inavyojiandaa michuano ya kimtaifa ya Caf.
“Nimegundua wapinzani wangu wananiogopa sana wakatengeneza Mtego tupoteze mechi 2 mfululizo wakafanikiwa na Wakaanza kuwajaza upepo viongozi wangu ili nifukuzwe,Bahati nzuri nina viongozi weledi zaidi ya akili zao mbovu wameziba masikio”Alisema Gamondi aliyechukua taji la ligi kuu na kombe la Shirikisho la Crdb nchini.
“Nami nasema hivi natoa material yote kwa klabu yangu ya Yanga sc hata kama ni kwa kutumia Gharama zangu binafsi ili niweze kuwafurahisha zaidi mashabiki wa Yanga na viongozi walionyesha ukomavu mkubwa”alimalizia kusema kocha huyo ambaye mabosi wa klabu hiyo bado wanamuangalia katika michezo ya kimataifa ili kufanya uamuzi wa kuendelea nae ama la.
Miguel Gamondi aliyejiunga na Yanga sc msimu uliopita akichukua nafasi ya Nasredine Mohamed Nabi ambapo alifanikiwa kuisaidia timu hiyo kuchukua kombe la ligi kuu kwa mara ya tatu mfululizo na kombe la Crdb la Shirikisho mara moja.