Connect with us

Soka

Gallagher aitwa England

Kiungo wa Chelsea Connor Gallagher ameitwa kwa mara ya kwanza kuitumikia timu ya Taifa ya Uingereza(Three Lions) baada ya timu huyo kukumbwa na majeruhi hivyo kulazimika kuwakosa nyota wake watano.

Gallagher amepewa imani hiyo na kocha mkuu Garry Southgate baada ya kuanza vizuri msimu huu kwa kufunga magoli manne na kutoa pasi za usaidizi(assisti) mbili akiwa na kikosi cha Crystal Palace kwa mkopo akitokea Chelsea.

England itacheza na San Marino siku ya Jumatatu katika mchezo wa mwisho kufuzu kombe la dunia Qatar ambao Taifa hilo linahitaji alama moja tu kuijhakikishia kufuzu michuano hiyo mikubwa kabisa ulimwenguni.

Southgate anatarajia kuwakosa nyota wake Jordan Henderson,Jack Grealish wamerudishwa kwenye vilabu vyao kwa matibabu zaidi huku Raheem Sterling akiukosa mchezo huo kwa sababu binafsi.

Wchezaji wengine Luke Shwa na Mason Mount walioukosa mchezo Ijumaa dhidi ya Albania hawatoweza tena kujiunga na timu hiyo kutokana na kushindwa kupona kwa wakati majeraha yanayowasumbua.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka