Connect with us

Makala

Fountain Gate Fc yailiza Coastal Union

Kocha Juma Mwambusi ana kazi ya kufanya baada ya kuishuhudia klabu yake ya Coastal Union ikikubali kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Fountain Gate Fc katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Tanzanite Babati Manyara.

Katika mchezo mkali na wa kusisimua Fountain Gate Fc ilipata bao la kwanza mapema dakika ya 16 likifungwa na Ellie Mukono lakini dakika ya 44 bao hilo lilisawazishwa na Lucas Kikoti kwa penati na lakini furaha hiyo haikudumu baada ya William Edgar kufunga bao la kwa Singida Fountain Gate Fc.

Dakika ya 54 ya mchezo huo Nicolaus Gyan aliipatia Fountain Gate Fc bao la tatu kwa penati na kuipa Coastal Union wakati mgumu lakini walirudi mchezoni na kupata bao la pili likifungwa na Maulid Maabad dakika ya 79 ya mchezo huo.

Baada ya kupata alama tatu muhimu sasa Fountain Gate Fc imefikisha alama 24 katika michezo 14 ya ligi kuu huku Coastal union ikisalia na alama 16 katika michezo hiyo hiyo 14.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala