Connect with us

Makala

Feisal,Azam Fc Kimeeleweka

Kiungo wa klabu ya Azam Fc Feisal Salum amekubali ofa ya USD 12,000 (Tshs 31.5m) ambao ni mshahara kutoka kwa mabosi wa klabu hiyo ili kusaini mkataba mpya wa miaka miwili na dola 320,000 (Tshs Milioni 841.8) ambao ni ada ya usajili.

Mabosi hao wanalazimisha dili hilo likamilike mapema ili kuzuia kiungo huyo fundi asijiunge na klabu zingine ambazo zinamnyemelea.

Mpaka sasa timu za Kaizer Chiefs chini ya kocha Nasredine Nabi na Simba Sc zote zimeonyesha nia ya kumsajili kiungo huyo zikifanya majaribio kadhaa.

Katika mkataba wake na Azam Fc katika mwaka wa mwisho wa mkataba dau lake litashuka hivyo Azam Fc inapambana kuhakikisha anasaini mkataba mapema kabla ya msimu huu kuisha.

Mpaka sasa katika ligi kuu nchini Feisal amechangia zaidi ya nusu ya mabao ya timu yake akifunga na kutoa asisti mara kadhaa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala