Connect with us

Makala

Feisal Atengewa Mamilioni Azam Fc

Taarifa kutoka ndani ya mabosi wa klabu ya Azam Fc zinasema kuwa wamejiandaa kumpa mkataba mpya kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Feisal Salum wenye mshahara wa shilingi milioni 40 kwa mwezi.

Mabosi hao wameamua kumpa mshahara huo mkubwa ili kumshawishi staa huyo kuongeza mkataba mpya baada ya huu wa sasa kubakisha mwaka mmoja mwishoni mwa msimu huu ambapo dau lake la usajili litashuka mpaka takribani milioni mita tano kutokana na vipengele vya mkataba wake wa sasa.

Klabu kadhaa za ndani ikiwemo klabu yake ya Yanga sc na Simba sc zimeonyesha ya kumsajili staa huyo huku Yanga sc ikiwa na nafasi zaidi kutokana na vipengele vya kimkataba kipindi inamuuza Azam Fc.

Inasemekana pamoja na kuwekewa mshahara huo bado Feisal hajasaini mkataba huo akihitaji zaidi ya kiasi cha shilingi milioni hamsini kwa mwezi ili kusalia klabuni hapo huku pia akiangalia zaidi ofa za nje ya nchi.

Azam Fc ilimnasa Feisal Salum kutoka Yanga sc usajili ambao ulileta mgogoro mkubwa baina ya mchezaji huyo na klabu hiyo kutokana na tafsiri ya Vipengele vya kimkataba.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala