Connect with us

Makala

Fadlu Afungukia usajili Simba sc

Kocha Mkuu wa klabu ya Simba Sc Fadlu Davis amesema kuwa anahitaji mastaa wapya klabuni humo lakini sio kujaza idadi bali watakaokua na msaada moja kwa moja kwenye timu hiyo.

Kocha huyo Raia wa Afrika ya kusini amesema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari siku ya jana ikiwa ni siku maalumu ya vyombo vya habari nchini kutembelea mazoezi na kambi ya klabu hiyo.

“Hatutosajili kwa kuongeza idadi ila kama watapatikana wachezaji bora zaidi ya tulionao tutasajili ila wakikosekana tutaendelea kuwapandisha ubora hawa waliopo”alisema Fadlu Davis

Pia kocha huyo alizungumzia usajili wa mshambuliaji Ellie Mpanzu “Tunahitaji wachezaji wapya waje kuingia kikosi cha kwanza moja kwa moja mfano Mpanzu ambaye ameonyesha utofauti mkubwa na washambuliaji waliopo ambapo ana ubora mkubwa wa kucheza nafasi zote za ushambuliaji”.

Fadlu mpaka sasa amefanikiwa kuirejesha klabu ya Simba Sc kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini ikifikisha alama 28 katika michezo 11 ya ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala