Connect with us

Soka

Dube Atinga TFF

Mshambuliaji Prince Dube ameenda katika shirikisho la soka nchini (TFF) akiwasilisha malalamiko yake akidai kwamba hatambui mkataba wake na klabu ya Azam Fc ambayo inadai kuwa ana mkataba wa miaka miwili na nusu na klabu hiyo.

Kwa mujibu wa Dube yeye anasema kuwa ana mkataba na klabu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu huu ambapo mkataba mpya wa miaka miwili ambao klabu hiyo inadai kuwa ilimsainisha kuwa hautambui na wala hajawahi kuusaini.

Malalamiko hayo ya Dube yanafanana kabisa na yale ya Benard Morrison ambaye aliukana mkataba wake na klabu ya Yanga sc na kufanikiwa nia yake kujiunga na klabu ya Simba sc ambayo ilimuwekea dau nono tofauti na lile la Yanga sc.

Azam Fc yenyewe inadai kuwa ina mkataba na staa huyo mpaka mwaka 2027 ambapo alisaini mkataba mpya mwishoni mwa msimu uliopita mkataba wa miaka miwili na kufanya jumla awe na mkataba wa miaka miwili na nusu.

Azam Fc ilitangaza kukaribisha ofa za vilabu mbalimbali vyenye nia ya kumsaini staa huyo lakini licha ya vilabu vya Simba sc na Al Hilal ya Sudan kujitokeza inadaiwa kuwa bado mchezaji huyo alikataa ofa hizo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka