Connect with us

Makala

Dube Amalizana na Azam Fc

Aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Azam Fc Prince Dube muda wowote atapewa barua ya kumalizana na klabu hiyo baada ya kufanikiwa kulipa zaidi ya shilingi milioni mia tano za kitanzania kwa ajili ya kulipa fidia ya kuondoka klabuni hapo.

Dube aliondoka Azam Fc katikati ya msimu akisema hautambui mkataba wake na klabu hiyo ambapo aliandika barua ya kuvunja mkataba wake uliosalia wa miezi sita huku akirudisha kila kitu alichopewa na Azam Fc.

Azam Fc wenyewe walibaki na msimamo wao kuwa kama anataka kuondoka basi analazimika kulipa zaidi ya shilingi milioni mia saba zilizopo katika mkataba wake ndipo awe huru au kama ana timu inamhitaji basi ilete ofa mezani.

Mgogoro huo ulisababisha kesi kupelekwa kamati ya maadili na hadhi za wachezaji (TFF) ambao waliamuru kuwa mchezaji huyo arejeshe fedha ya usajili aliyochukua kwa ajili ya mkataba mpya uliokua unaisha mwaka 2026 huku pia akitakiwa kulipa fidia kutokana na kutoutumikia mkataba wake unaoisha msimu huu kikamilifu.

Taarifa zinasema kuwa tayari amesharejesha kiasi hicho kupitia benki na sasa anasubiri barua ya kumuachia huru (Release Letter) kutoka kwa mabosi wa klabu hiyo ili ajiunge na timu nyingine hapa nchini ambapo mchezaji mwenyewe amethibitisha hilo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala