Connect with us

Soka

Dante,Abdul Wapigwa “Stop” Yanga

Inaelezwa kuwa mabeki wa timu ya Yanga sc Juma Abdul na Andrew Vicent “Dante” wamesimamishwa na uongozi wa klabu hiyo kwa muda usiojulikana baada ya kutoripoti kambini mjini Morogoro kwa muda mrefu.

Habari za ndani zinadai wachezaji hao wamegoma kushinikiza kulipwa madai yao ya fedha za usajili na mishahara wanazodai klabuni hapo baada ya kuongeza mikataba mwaka jana na mwaka juzi hali iliyowalazimu kugoma kuripoti kambini baada ya uongozi kutotimiza ahadi yao ya kuwalipa kabla ya msimu mpya kuanza huku wale wachezaji wa kigeni wakitimiziwa stahiki zao zote.

Mmoja ya wachezaji hao alidai wamegoma ili watimiziwe mahitaji hayo ndio wajiunge kambini kama wenzao,Mabeki hao hawajaripoti kambini sambamba na mkongwe Kelvin Yondani huku taarifa zikidai Yondani ana ruhusa maalumu kutoka kwa uongozi wa klabu hiyo ili kushughulikia.

Taarifa zinadai uongozi wa klabu hiyo umeamua kuwasimamisha wachezaji kwa muda usiojulikana baada ya kuonesha utovu wa nidhamu kwa kutoripoti kambini na kuhusu madai yao uongozi ungeshughulikia huku wakiwa kambini na sio kuripoti katika vyombo vya habari.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka