Connect with us

Makala

Man Utd Balaa

Kikosi cha Manchester United kimeendelea kuonyesha makali katika michuano ya Icc baada ya jana kuifunga timu ya Tottenham kwa mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika nchini China.

Athony Martial ameendelea kuonyesha kuwa anastahili kuanza katika nafasi ya mshambuliaji wa kati baada ya kuipatia united bao la kuongoza akimalizia vizuri pasi ya kupenyeza kutoka kwa Andres Pereira bao lililodumu mpaka kipindi cha pili baada ya Lucas Moura kuzawazisha kupitia shuti lililomgonga beki wa manchester na kubadili uelekeo na kumuacha kipa wa Sergio Romero asijue cha kufanya.

Mabadiliko yaliyofanywa na makocha wote yalikua na tija isipokua uwepo wa makinda wenye kasi ilikua chachu ya ushindi kwa united baada ya kinda Angel Gomez kuipatia timu hiyo bao la pili baada ya kugongeana na Mata mbele ya msitu wa wachezaji wa Spurs na kufanya mechi hiyo kumalizika kwa united kuibuka na ushindi.

Katika mchezo beki Erick Bailly aliumia na kutolewa mchezoni na kwenda kutibiwa japo haijajulikana ukubwa wa jeraha mpaka afanyiwe uchunguzi wa kina hivyo hali hiyo inamlazimu kocha Solskjaer kuharakisha usajili wa Harry Maguire kuja kuziba nafasi hiyo ikizingatiwa beki huyo ametoka kuikosa michuano ya Afcon kwa majeruhi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala