Connect with us

Makala

Coastal Union Yashusha Straika Mmali

Klabu ya Coastal Union ya Jijini Tanga imesajili mshambuliaji Amara Bagayoko raia wa Mali ili kuongeza ufanisi katika safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 26 amesajiliwa akitokea katika ligi kuu ya Togo ambapo alikua amefunga jumla ya mabao 19 katika ligi hiyo.

Usajili huo umepitishwa na kocha Juma Mwambusi ambapo umelenga kuongeza ufanisi wa ufungaji ambapo katika michezo 15 ya ligi kuu ya Nbc nchini klabu hiyo imefunga mabao 15 pekee.

Staa huyo baada ya kusaini mkataba mfupi mpaka mwisho wa msimu huu tayari ameshawasili jijini Arusha ilipo kambi ya klabu hiyo tayari kwa michezo ijayo ya ligi kuu ya Nbc nchini.

Katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini klabu hiyo imecheza michezo 15 ikiwa katika nafasi ya 10 ikiwa na alama 17 pekee.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala