Connect with us

Makala

Chama,Yao Kuwakosa Tp Mazembe

Mastaa Yao Kouasi Attouhoula na Cletous Chama wanatarajiwa kuukosa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Tp Mazembe unaofanyika leo katika uwanja wa Benjamin Mkapa kutokana na majeraha yanayowakabili.

Chama ambaye anasumbuliwa na jeraha la mkono ambapo ameumia kiwiko huku Yao akisumbuliwa na jeraha la goti.

Meneja wa Idara ya habari ya klabu ya Yanga sc Ally Kamwe amesema kuwa wachezaji hao wamepona kwa zaidi ya asilimia hamsini lakini wameamua kuwaweka pembeni ili wapone vizuri zaidi.

“Sisi tuna utajiri wa wachezaji ndio maana tumeona wapumzike ili wapone vizuri zaidi kwa maana msimu ndio kwanza upo katikati na bado kuna mechi nyingi”.Alisema Kamwe akizungumza kupitia kipindi cha michezo cha radio Crown Fm.

Yanga sc inashuka leo katika mchezo wa kuamua hatma yake ya kuendelea kuweka matumaini ya kufuzu robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika ama lah.

Mpaka sasa Yanga sc iko mkiani mwa msimamo ikiwa na alama moja na endapo ikishinda basi itafikisha alama nne zitakazotoa matumaini ya kufuzu robo fainali ya michuano hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala