Connect with us

Makala

Chama,Diarra Kuwakosa Mashujaa Fc

Klabu ya Yanga sc ikielekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc imetangaza kuwakosa mastaa wake Djigui Diarra sambamba na Cletous Chama kutokana na kusumbuliwa na majeraha waliyoyapata katika mchezo uliopita dhidi ya Tp Mazembe.

Mchezo utakaofanyika leo katika uwanja wa Kmc Complex Jijini Dar es Salaam ambapo Yanga sc inapaswa kushinda ili kurejesha imani kwa mashabiki wa klabu hiyo kutokana na kutopata matokeo mazuri katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika kama alivyosema kocha Sead Ramovic.

“Tunapewa nafasi ya kufanya vizuri lakini hilo halitufanyi tuwadharau wapinzani wetu, tunajiandaa vizuri kuhakikisha wachezaji wanakwenda kufanyia kazi tunayowaelekeza mazoezini. Tunaamini utakuwa mchezaji mzuri wenye ushindani”.

Hata hivyo mastaa hao wamekua muhimu kikosini humo kutokana na mchanga wao katika michezo ya ligi kuu hivi karibuni.

Uwepo wa Stephen Aziz Ki pamoja na AbouTwalib Mshery na Abubakar Khomeini ndio unampa ahueni kocha Ramovic kuwa wanaweza kuziba mapengo hayo.

Mpaka sasa katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini Yanga sc imecheza michezo 11 ikiwa na alama 28 katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala