Connect with us

Makala

“Bravos Sio Wepesi”Mohamed Hussein

Staa wa klabu ya Simba Sc Mohammed Hussein amesema kuwa mchezo dhidi ya timu ya Bravos ya Angola sio rahisi kutokana na timu hiyo kuwa na wachezaji wazuri.

Hussein amesema hayo alipokua uwanja wa ndege wakati wakirejea kutoka nchini Tunisia walipocheza na timu ya Sc Sfaxien na kupata ushindi wa 1-0 na kufikisha alama tisa katika nafasi ya pili ya msimamo wa kundi A la michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

“Mchezo wetu dhidi ya Bravos utakua mgumu sana kwa sababu wao wametoka kupoteza kwahiyo na wao jicho lao litakua katika mchezo huo lakini sisi pia tunahitaji matokeo kwenye mchezo huo kuhakikisha tunajiweka katika nafasi nzuri kwenye kundi hilo”.Alisema Hussein

“Wachezaji tunaamini tutapambana na kuhakikisha tunapata matokeo kwenye mchezo huo”.Alimalizia kusema staa huyo ambaye ni nahodha wa kikosi hicho.

Simba sc itapambana na Bravos siku ya Jumapili Januari 12 ambapo ikipata ushindi basi moja kwa moja itakua imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala