Connect with us

Makala

Boka Afiwa na Baba Mzazi

Mchezaji wa Klabu ya Yanga sc Shadrack Boka amefiwa na baba yake mzazi msiba uliotokea juzi tarehe 11/01/2025 huko nyumbani kwao Jijini Kinshasa nchini Congo Drc.

Taarifa za kifo chake zimetolewa na Uongozi wa Klabu yake ya Yanga Sc katika mitandao ya kijamii ya klabu hiyo.

“Uongozi wa Young Africans Sports Club tunapenda kutoa pole kwa mchezaji wetu Chadrack Boka, kufuatia kifo cha Baba yake Mzazi kilichotokea Tarehe 11/01/ 2025, nyumbani kwao Kinshasa DR Congo”,Zilisomeka taarifa hizo.

“Uongozi wa Young Africans unaungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na unawataka wanafamilia wote kuwa na subira”,Ilimalizia kusomeka taarifa hiyo.

Hata hivyo taarifa hiyo haikumzuia beki huyo kucheza mchezo wa tarehe 12 dhidi ya timu ya Al Hilal Omdurman uliofanyika nchini Mauritania na klabu hiyo kupata ushindi.

Tayari staa huyo ameelekea nchini Congo Dr kwa ajili ya mazishi na anatarajiwa atarejea nchini kwa ajili ya mchezo unaofuatia dhidi ya Mc Algers utakaofanyika hapa nchini Januari 18.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala