Connect with us

Soka

Benchika Rasmi Aondoka Simba sc

Klabu ya Simba sc imethibitisha kuachana na  kwa kocha Abdelhack Benchika pamoja na wasaidizi wake klabuni hapo kutokana na matatizo ya kifamilia ambayo yamilazimu klabu hiyo kukubaliana kuachana na kocha huyo.

Benchika aliuomba uongozi kuachia ngazi ili apate nafasi ya kuwa karibu na mke wake ambaye ni mgonjwa hivyo kuhitaji uangalizi wa karibu wa mume wake ambapo klabu hiyo imekubaliana na ombi hilo na kutoa taarifa rasmi kwa umma kuachana na kocha huyo aliyekua anatarajiwa kufanya makubwa klabuni hapo.

Kabla ya taarifa ya klabu hiyo tayari kulikua na tetesi za Benchika kupanga kuachana na klabu hiyo msimu ukiisha kutokana na kutofautiana na uongozi wa klabu hiyo katika mambo mengi ya msingi hasa kuhusu usajili mpya wa wachezaji katika dirisha dogo la mwezi januari ambapo mastaa kadhaa aliowahitaji kocha huyo alishindwa kupatiwa.

Pia mshahara mkubwa aliokua analipwa kocha huyo ni moja ya sababu ya klabu hiyo kukubali kuachana nae kutokana na ukweli kwamba gharama za kummiliki zilikua kubwa tofauti na uwezo wa klabu hiyo.

Taarifa zaidi zinasema kuwa tayari kocha huyo ana ofa kadhaa zikiwemo kutoka klabu za Al Ahly Fc,Zamalek Fc pamoja na timu za Taifa za Algeria na Mauritania huku klabu za Cr Belouzdad na Wydad Ac zikiwa pia zinamtolea macho.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka