Connect with us

Soka

Barcelona,Man Utd zapigwa Ulaya

Klabu za Barcelona na Manchester United zimeanza vibaya kwa kupoteza michezo yao ya kwanza ya makundi ya klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Byern Munich na Young Boys.

Barcelona waliokuwa katika dimba la Nou Camp walivurumishwa kwa mabao 3-0 na ,mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich.Mabao ya Bayern yaliwekwa kambani na Thomas Muller dakika ya 34 na mengine yakifungwa na Robert Lewandowski dakika ya 56 na 85.

Upande wa Man Utd waliokuwa Uswisi walipoteza kwa 2-1 dhidi ya wenyeji Young Boys katika mchezo ambao walicheza pungufu kwa muda mrefu baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu beki Aaron Wan Bissaka.Cristiano Ronaldo licha ya timu yake kupoteza bado aliifungia timu yake bao pekee.

Matokeo mengine ya ligi hiyo usiku wa jana ni kama ifuatavyo;

Chelsea 1-0 Zenit St Petersburg

Sevilla 1-1 RB Salzburg

Villareal 2-2 Atalanta

Dynamo Kyv 0-0 Benfica

Malmo 0-3 Juventus

Lille 0-0 Wolfsburg

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka