Connect with us

Makala

Aziz Ki Mguu Nje Yanga Sc

Inaelezwa kuwa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Stephane Aziz Ki yupo mbioni kuondoka katika klabu hiyo baada ya kupata ofa kutoka takribani timu nne Barani Afrika.

Klabu za Orlando Pirates, MC Alger, Wydad Casablanca na Al Ahly Benghazi zinawinda saini ya kiungo wa huyo Stephan Aziz K raia wa Burkina Faso.

Ki msimu uliopita alisaini mkataba mpya katika klabu yake ya Yanga Sc na hivyo uamuzi wa kuondoka upo mikononi mwa klabu yake endapo itakua tayari kumuuza japo yeye mwenyewe tayari anafikiria maisha nje ya klabu hiyo.

Tayari Kuna taarifa kadhaa zimekuwa zikiekeza kuwa huenda nyota huyo akataka kwenda kujaribu Changamoto mpya sehemu nyingine baada ya kuitumikia Yanga SC Kwa takribani miaka mitatu.

Pamoja na Ki tayari bosi wa klabu hiyo Eng.Hersi Said alithibitisha kuwa kuanzia mwishoni mwa msimu huu wako tayari kuanza kusikiliza ofa za wachezaji wake mbalimbali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala