Connect with us

Soka

Aziz Ki Bora Machi 2024

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Stephane Aziz Ki ameibuka  kuwa mchezaji bora mwezi Machi msimu wa ligi kuu kwa msimu wa baada ya kutangazwa na bodi inayosimamia ligi kuu nchini kupitia kamati yake maalumu ya Tathmini ya viwango vya wachezaji 2023/2024.

Aziz KI amechukua tuzo hiyo mbele ya Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam FC na Clatous Chama wa Simba alioingia nao fainali kwenye mchakato huo kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyotangazwa hivi karibuno

Ki amechukua tuzo hiyo kutokana na kuwa ameisaidia timu yake kupata ushindi katika michezo mitatu kati ya minne waliyocheza huku akifunga mabao matatu na asisti nne, hivyo kuifanya klabu yake kupata pointi tisa na kusalia kwenye nafasi ya kwanza ya msimamo wa Ligi Kuu.

Hii ni mara ya pili kwa msimu huu Aziz KI anachukua tuzo ya mchezaji bora, mara ya kwanza alichukua mwezi Oktoba mwaka jana.

Msimu huu staa huyo amekua na kiwango kikubwa tangu ajiunge na Yanga sc ambapo mpaka sasa amefunga jumla ya mabao 13 katika ligi kuu nchini huku akikosa mechi kadhaa kutokana na kuchelewa kurudi kutoka timu ya Taifa ya Burkina Faso ambapo alienda kwenye michuano ya Afcon 2023.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka