Connect with us

Soka

Aziz Ki Aibuka Mfungaji Bora Ligi Kuu

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Stephane Aziz Ki ameibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya soka ya Nbc nchini Tanzania baada ya kufunga jumla ya mabao 21 na kumpiku Feisal Salum mwenye mabao 19 ya ligi kuu nchini iliyotamatika rasmi siku ya Mei 28 mwaka huu.

Aziz Ki amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao matatu “Hattrick” katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons uliofanyika katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam na kuisaidia klabu yake ya Yanga sc kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.

Licha ya Feisal Salum kuonyesha ushindani wa hali ya juu huku akifunga katika ushindi wa 2-0 wa klabu yake dhidi ya Geita Gold Fc na kufikishia mabao 19 ambayo hayakutosha kumpa tuzo hiyo baada ya Hattrick ya  Aziz Ki katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam.

Msimu huu wa ligi kuu umekua na mabadiliko makubwa katika eneo la ufungaji ambapo viungo ndio wameibuka kidedea badala ya washambuliaji wa asili ambapo Waziri Junior wa Kmc ndie pekee amefikisha mabao 12 katika washambuliaji wa asili kabisa tofauti na misimu miwili iliyopita ambapo Fiston Mayele,George Mpole na Prince Dube walifanya vizuri.

Msimu huu umekua bora sana kwa Stephane Aziz Ki ambapo pia licha ya kuwa mfungaji bora pia ametoa asisti nyingi za mabao kwa timu yake na ligi kwa ujumla  ambapo akitoa assisti nane nyuma ya Kipre Junior mwenye tisa na Feisal Salum anazo saba na kuweka ugumu kwa klabu yake ya Yanga sc kumuongezea mkataba kutokana na kuwa na ofa nyingi zaidi na bora kutoka kwa timu bora barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka