Connect with us

Soka

Azam Wala Kibano TFF

Klabu ya Azam FC imetozwa faini ya Tsh 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la timu hiyo kuchelewa kutoka uwanjani hata Kamishna alipowaita walikaidi amri ya kutoka vyumbani na golikipa wa timu hiyo kuchelewa zaidi na alipofika uwanjani kushindwa kuwapa mikono timu pinzani (Coastal Union) kwenye mchezo uliofanyika February 15, 2020 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(43) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo ambapo kosa hilo lilitendeka katika Mechi namba 218- Azam FC 1 vs Coastal Union FC 2 mchezo uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka