Connect with us

Soka

Corona Yasimamisha Serie A

Baadhi ya mechi ambazo zilitakiwa kupigwa leo nchini Italia zimehairishwa kutokana na hofu juu ya Virusi vya Corona ambavyo vinasambaa kwa kasi duniani.

Taarifa kutoka ESPN zinasema kwamba mechi ambazo zilitakiwa kupigwa katika mikoa ya kaskazini Lombardy na Veneto , kati ya Inter Milan dhidi ya Sampdoria, Sassuolo dhidi ya Atalanta na Hellas Verona dhidi ya Cagliari zote zimehairishwa .

ESPN wameripoti kwamba miji mingi katika ukanda wa Kaskazini mwa Italia imefungwa baada ya vifo vya watu wawili walioathirika na Virusi vya Corona .

Ugonjwa huo ulianzia nchini china na unadaiwa usambaa baadhi ya nchi duniani ambapo mpaka sasa inasemekana zaidi ya watu 1000 wamefariki nchini China Pekee.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka