Connect with us

Makala

Azam Fc Yamtambulisha Staa wa Mali

Klabu ya Azam Fc imemtambulisha winga mshambuliaji Cheickna Diakite, akitokea katika klabu ya  soka ya Real Bamako inayoshiriki ligi kuu nchini Mali ambapo amesaini mkataba wa miaka mitatu kukaa Chamazi Complex mpaka mwaka 2027.

Diakite ni mshambuliaji anayetokea pembeni akisifika zaidi kwa kasi na chenga za maudhi huku akiwa na nguvu za kutosha kuisumbua ngome ya timu pinzani kwa dakika zote 90 za mchezo hasa ikichagizwa na umri wake wa miaka 19.

Azam Fc iliwapasa kufanya kazi ya ziada kumnasa staa huyo ambaye alikua na ofa kutoka klabu kadhaa za kaskazini mwa Afrika ambazo zina nguvu kubwa kiuchumi sambamba na baadhi ya klabu barani ulaya hasa Ufaransa ambazo nazo zilivutiwa na uwezo wa staa huyo.

Mshambuliaji huyo amesajili kuchukua nafasi ya Kipre Jr ambaye ameuzwa kwa zaidi ya dola za kimarekana laki mbili kwenda katika klabu ya Usm Algers ya nchini Algeria na kuwafanya mabosi wa klabu hiyo kutafuta mbadala wake haraka ili isilete athari kwenye timu baada ya msimu uliopita Kipre Jr kufunga mabao 9 na kusaidia upatikanaji wa mabao 9 katika ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala