Klabu ya soka ya Azam Fc ya jijini Dar es salaam imetangaza kujitoa katika michuano ya soka ya Kagame Cup inayotarajiwa kufanyika nchini Tanzania Visiwani Zanzibar kuanzia Julai 6 mwaka huu katika uwanja wa Amani Visiwani Zanzibar.
Akitangaza uamuzi huo Meneja wa Idara ya habari ya klabu hiyo Zakaria Thabit alisema kuwa timu hiyo haitashiriki michuano hiyo kutokana na ratiba ya michuano hiyo kuingiliana na ratiba ya maandalizi ya msimu mpya wa 2024/2025.
“Azam Fc haitoshiriki michuano hiyo ya Kagame kutokana na timu kuwa kwenye mapumziko mpaka tarehe 4 julai ndipo wachezaji watarejea kuanza pre seasons,Tarehe hizo zitakuwa ngumu kwetu kutokana na wachezaji wote wanatakiwa kukaa press session zaidi ya wiki sita na hii kwa mujibu wa kitalaamu timu iwe tayari kwa mashindano ”amesema Meneja habari Azam FC Zakaria Thabit maarufu kama Zaka Zakazi.
Awali michuano hiyo ilipangwa kufanyika nchini Sudan lakini kutokana na hali ya kisiasa kutotengemaa basi iliwalazimu Cecafa kuihamishia michuano hiyo Zanzabar huku Sudan wakipewa nafasi ya kuingiza timu nne kama mwenyeji ambapo timu za El Merreikh, Al Hilal, Hai El Wadi zitashiriki huku Tanzania ikiingiza timu za Simba sc,Yanga sc,Azam Fc na Coastal union na Rwanda ikiingiza timu ya APR na Vital O kutoka nchi ya Burundi itashiriki.
Timu nyingine ni Gor Mahia (Kenya), SC Villa (Uganda), JKU SC (Zanzibar), El Merreikh FC-Bentiu (Sudan Kusini), Nyasa Big Bullets (Malawi), TP Mazembe (DR Congo) na Red Arrows (Zambia) ambazo zitaungana na timu alikwa kuunda timu 16 zitakazoshiriki michuano hiyo inayodahminiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame.