Connect with us

Soka

Azam Fc Yajichimbia Kileleni Nbc

Klabu ya Azam Fc Imejichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini baada ya kuifunga Singida Fountain Gate kwa mabao 2-0 na kufikisha alama 33 kileleni mwa msimamo.

Katika mchezo uliofanyika Disemba 17 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam Azam Fc ilipata mabao yake dakika ya 31 likifungwa na Gibril Sillah aliyemalizia kazi nzuri ya Feisal Salum sambamba na bao la dakika za nyongeza ya Allasane Diao aliyemalizia kona nzuri ya Lusajo Mwaikenda.

Azam Fc sasa imefikisha alama 33 kileleni mwa msimamo ikicheza michezo 15 ya ligi kuu ya Nbc huku Singida Black Stars ikiwa nafasi ya pili ikiwa na alama 28 ikicheza mechi 14.

Azam Fc inapaswa kuziombea Simba sc na Yanga sc zipoteze baadhi ya michezo yake ili iendelee kukaa kileleni ambapo timu hizo mpaka sasa zimecheza michezo 11 pekee ya ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka