Connect with us

Soka

Azam Fc Yaizamisha Mtibwa Sugar

Klabu ya Azam Fc imezidi kuzamisha jahazi la Mtibwa Sugar baada ya kuichapa mabao 2-0 ugenini katika uwanja wa Manungu Complex ulioko Turiani Morogoro katika mchezo wa ligi kuu ya soka ya Nbc uliofanyika Mei 06 2024.

Azam Fc ikianza na kikosi chake cha kila siku ilianza kupata bao dakika ya 20 baada ya krosi iliyopigwa na Ayoub Lyanga kupigwa kichwa na Dan Amoah ambaye alipiga kichwa kilichopanguliwa na kipa Mohamed Makaka na mpira kumkuta Feisal Salum ambaye aliutia nyavuni.

Licha ya Mtibwa kujitahidi kusawazisha bao hilo kipindi cha pili waliadhibiwa tena kwa shambulizi la kushtukiza ambapo mpira wa krosi ya chinichini ya Feisal Salum ulimkuta Gibril Silla ambaye alimchungulia kipa Makaka na kuandika bao la pili.

Azam Fc sasa wamefikisha alama 57 nyuma ya Yanga sc iliyo kileleni na alama 65 baada ya timu zote kucheza michezo 25 ya ligi kuu huku Mtibwa Sugar ikiwa mkiani mwa msimamo na alama 17 katika michezo 25 ya ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka