Connect with us

Makala

Azam Fc Yailaza Apr 1-0

Klabu ya Azam Fc imeanza michuano ya kombe la Klabu bingwa barani Afrika kwa ushindi kiduchu wa 1-0 dhidi ya Apr ya Rwanda katika mchezo wa hatua ya awali ya michuano hiyo uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

Ikianza na kikosi chake kinachoonekana ndio cha kwanza kikiwa na mastaa kama Mohammed Mustapha,Paschal Msindo,Lusajo Mwaikenda huku Yanick Bangala na Yeison Fuentes wakiwa kama mabeki wa kati na kiungo kikiongozwa na Adolph Mtasingwa Bitegeko na James Akaminko waliosaidia na Frank Tiesse na Gibril Sillah huku washambuliaji wakiwa ni Feisal Salum na Jhonier Blanco.

Azam Fc sambamba na kuwa na kikosi hicho bado walishindwa kupata bao lolote katika dakika 45 za kupindi cha kwanza huku wakipaswa kumshukuru kipa Mohammed Mustapha kwa kuokoa hatari kadhaa kutokana na mashambulizi ya kushtukiza kutoka kwa Apr.

Feisal Salum alifanyiwa madhambi dakika ya 56 na mwamuzi kuamuru penati iliyopigwa kiufundi na Jhonier Blanco dakika ya 56 na kuipatia Azam Fc bao pekee katika mchezo huo.

Dakika tisini za mchezo huo zilitamatika kwa ushindi huo huku kibarua kikihamia jijini Kigali ambapo utapigwa mchezo wa marudiano wikiendi ya August 25 ambapo mshindi atavaana na mshindi baina ya Pyramid Fc dhidi ya Kvz ya visiwani Zanzibar.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala