Connect with us

Makala

Aucho Aifungukia Azam Fc

Kiungo wa klabu ya Yanga sc Khalid Aucho amesema kuwa mchezo baina ya klabu hiyo na Azam Fc ndio mechi pekee ambayo humsumbua yeye binafsi kutokana na timu ya Azam Fc kucheza kwa kukamia tofauti na michezo mingine wanayocheza.

Kiungo huyo raia wa Uganda na nahodha wa timu ya Taifa ya nchi hiyo amesema hayo mchana wa leo Disemba 27 alipokua alifanya mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni siku ya vyombo hivyo kuzungumza na mastaa wa klabu hiyo (Media day).

“Mechi yangu Bora ambayo huwa ina upinzani mkubwa Tanzania ni Azam Fc wakicheza na Yanga sc huwa wanapambana sana kama ni Champions League nadhani mechi nyingine wakiwa wanapambana kama wanavyo cheza na Yanga Basi watakua ni Mabingwa wanatimu nzuri wanatupatia mechi ngumu tukicheza nao”.Alisema Aucho kwa msisitizo.

Miaka ya hivi karibuni mchezo baina ya timu hizo umekua na ushindani mkubwa ambapo unakaribiana na ule unaozikutanisha Simba sc dhidi ya Yanga sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala