Connect with us

Makala

Ateba Aimaliza Pamba Jiji Fc

Bao la penati dakika ya 23 la Lionel Ateba limeiwezesha klabu ya Simba Sc kuchukua alama tatu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Klabu ya Pamba Jiji uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza.

Ateba alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi ya Awesu Awesu na beki wa Pamba Jiji Fc kumchezea faulo wakati akitazamana na kipa Yona Amos na ndipo mwamuzi alipoamuru pigo huru la mkwaju wa penati.

Mchezo huo uliotawaliwa na mambo mengi ya nje ya uwanja tangu Simba sc ilipowasili jijini humo ambapo hali hiyo imesababisha shauku kubwa kwa mashabiki na vyombo vya habari ikijumlisha pia vyombo vya dola.

Kutokana na hayo ya nje ya uwanja,ndani ya uwanja Mchezo huo ulikua wa kasi huku kila upande ukijitahidi kupata ushindi.

Simba sc sasa baada ya kuchukua alama tatu muhimu imefanikiwa kufikisha alama 28 kileleni mwa msimamo huku kwa upande wa wenyeji hali ikizidi kuwa tete kwani wamesaliwa na alama 8 pekee wakiwa wa pili kutoka mkiani licha ya kucheza michezo 12 mpaka sasa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala