Connect with us

Makala

Adam Adam Arejea Azam Fc

Klabu ya Azam Fc imemrejesha klabuni hapo mchezaji Adam Adam kutoka Mashujaa Fc ikiwa imepita miaka 10 tangu aitumikie akademi ya klabu hiyo mwaka 2014 katika michuano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

Mabosi wa klabu hiyo wameamua kumsajili mchezaji huyo kama usajili huru baada ya kumaliza mkataba na Mashujaa Fc na kuja kuungana tena na waajiri wake wa zamani akiwa kinda wa chini ya miaka 17 ambapo amesaini mkataba wa mwaka mmoja ukiwa na kipengele cha kuongeza mwingine endapo ataonyesha nidhamu na kiwango.

“Tunathibitisha kuwa tumeingia naye mkataba wa mwaka mmoja, tayari kabisa kuitumikia Azam FC msimu ujao 2023/24 ,dam Adam msimu uliopita alifanikiwa kufunga jumla ya mabao saba kwenye ligi, alipokuwa na kikosi cha Mashujaa”.Ilisomeka taarifa ya klabu hiyo kwenda kwa umma ikimtambulisha mchezaji huyo.
Mshambuliaji huyo ni moja ya zao la Akademi ya Azam FC, aliyojiunga nayo mwaka 2011-2014, ikiwa chini ya kocha Mhindi, Vivek Nagul na kubeba baadhi ya mataji kama vile U-20 Uhai Cup na Rollingstone.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala