Klabu ya Simba sc imethibitisha kuwa inahitaji takribani kiasi cha zaidi ya shilingi za kitanzania bilioni mbili ili kuamuachia staa wake Kibu Dennis kujiunga na klabu ya Kristiansund BK ya nchini Norway ambayo imeanza mchakato wa kumfanyia majaribio bila kufuata utaratibu sahihi.
Klabu hiyo ilimtumia Viza na tiketi ya ndege staa huyo kwenda nchini humo kwa majaribio bila kuwasiliana na klabu yake ya Simba sc ambayo ina mkataba na staa huyo aliousaini muda si mrefu wenye thamani ya kiasi cha shilingi bilioni 2.7 ili kuuvunja kwa mujibu wa makubaliano.
Klabu hiyo inashiriki ligi daraja la kwanza nchini Norway imehitaji kumsajili moja kwa moja staa huyo lakini ikiomba kupunguziwa bei kwa maana haina uwezo wa kumsajili moja kwa moja kwa dau tajwa huku uongozi wa juu wa Simba sc ukiweka ngumu.
“Tumeona na kusikia upande wa mchezaji ukijaribu kutushawishi tumuuze kwenda Norway kwa bei wanayoitaka wao jambo ambalo sio sawa na linazidi kumuweka huyo mchezaji matatizoni na msimamo wa klabu haujabadilika wa kuitaka klabu hiyo imnunue mchezaji moja kwa moja kwa dau la dola milioni moja na sio kufanya majaribio”Kilimalizia kusema chanzo hicho makini kutoka katika ngazi za juu za klabu hiyo
Mpaka sasa inasemekana kuwa mchezaji huyo amekwama katika majaribi0 hay0 na amerejea nchini kuiomba klabu hiyo imruhusu ajiunge na kambi ya maandalizi ya msimu mpya huku akikiri makosa yake na mpaka sasa bado uongozi huo haujatoa tamko rasmi kuhusu hilo.