Connect with us

Riadha

Semenya Aibuka Kidedea Ufaransa

Mwanariadha wa kike kutoka Afrika ya Kusini Caster Semenya ameibuka mshindi katika mbio za mita 2,000 zilizofanyika jijini Paris Ufaransa ukiwa ni ushindi wake wa kwanza tangu awasilishe rufaa yake dhidi ya IAAF kupinga sheria ya kumtaka apunguze homoni ili zifanane na wanariadha wengine wa kike.

Semenya mwenye miaka 28 alitumia dakika 5 na sekunde 38.19 dhidi ya muethiopia Hawi Feysa na Adanech Anbesa jijini Paris

“Nina kipaji na sina wasiwasi,ninaweza kukimbia mbio zozote ziwe za mita 200,300 au mbio ndefu” alisema mwanariadha huyo ambaye amekata rufaa katika mahakama ya juu nchini uswisi baada ya kushindwa kesi katika mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo mwezi uliosha dhidi ya sheria mpya inayomtaka staa huyo kupunguza homoni zake ili kushindana katika mbio za mita 800 au kubadili mbio.

Semenya mshindi mara mbili wa michuano ya olympic huku akitwaa ubingwa wa dunia mara tatu ametajwa katika kikosi cha riadha cha timu ya taifa ya Afrika kusini itakayoshiriki michuano ya riadha ya Doha  ya mita 800 baadae mwaka huu,ushiriki wake utategemea na matokeo ya rufaa yake amesisitiza yeye sio muongo bali ni mwanariadha halisi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Riadha